This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha Bandara - Premiumbloggertemplates.com.

TAMKO LA DCPC JUU YA MWANDISHI KUPIGWA RISASI

Sunday, December 9, 2012


Kufuatia kupigwa risasi,  kujeruhiwa begani na kulazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama hai wa Dar City Press Club(DCPC), uongozi wa Klabu uliamua kufuatilia tukio hilo kwa karibu ili kujua na kuhakiki kwa kina yaliyotokea na sababu zilizopelekea hayo kutokea.
Kutokana na hayo DCPC imebaini yafuatayo.
1.      Ni kweli kwamba Shabaan matutu(30) alipigwa risasi na askari wa jeshi la Polisi mwenye namba F.8991 D/C Idrissa nyumbani kwa Shabaan kimakosa baada ya askari huyo na wenzake wanne kufungua kwa nguvu na bila ya kujitambulisha kwa mwenye nyumba (Shabaan na Mkewe) licha ya kuombwa kufanya hivyo kabla.
2.      Kuna maelezo yanayokinzana katika kuelezea jinsi tukio hilo lilivyotokea kwa pande mbili zinazohusika yaani maelezo ya shabaan na ya polisi.
3.      Kwamba sababu za askari polisi hao kufanya hivyo hazikuwa zimefanyiwa uchunguzi wa kutosha hadi kujiridhisha kuchukua hatua hiyo hivyo hata wao walikiri kukosea pamoja na kueleza kwamba Shabaan ndiye aliyeaanza kuwashambulia askari Polisi kabla ya wao kumjeruhi kwa risasi.
4.      Shabaan mpaka sasa anaendelea na matibabu licha ya kuuguza majeraha aliyosababishiwa na polisi na kwamba ameshauriwa kitaalamu kupumzika nay eye binafsi ameomba asibughudhiwe ili afya yake irejee
haraka na kwamba pindi atakapokuwa katika hali nzuri zaidi ya sasa kwa mujibu wa ushauri huo wa kitabibu, atawasiliana na yeyote wakiwemo polisi ambao  wamekuwa wakimmghasi kwa kuja kumhoji mara kwa mara.

Kwa sababu hizo basi Dar es salaam City Press Club
1.      Tunaiomba Serikali na mamlaka za juu zaidi ya jeshi la Polisi hususan Wizara ya mambo ya ndani ifanye uchunguzi wa kina na huru wenye kuhusisha taasisi wakilishi katika jamii juu ya tukio hilo na
kulichunguza jeshi la polisi linavyofanya kazi zake kwa kuzingatia kanuni na sheria.
2.      Tunalitaka Jeshi la Polisi liache mara moja kutuma askari wake kwenda kwa Shabaan kwa lengo la kumhoji ama kutaka atoe maelezo yake kwa viongozi wa jeshi hilo ilhari walishamtuhumu na kueleza kuwa
aliwashambulia Polisi kwa Panga kabla ya wao kumfyatulia risasi.Tunasema hivi kwa kuzingatia kanuni za afya na haki za msingi za binadamu.
3.      Tunalitaka Jeshi la Polisi liueleze umma bila kuficha ukweli na kwa jinsi ile ile ambayo lilitoa taarifa mara baada ya tukio, lieleze kwa nini linatumia habari na vyanzo dhanifu kujeruhi na kuhatarisha maisha ya raia wasio na kosa huku likitoa maelezo yasiyofanyiwa uchunguzi.
4.      Mwisho tunalitaka jeshi la Polisi lenyewe lijitafiti na kujipanga upya ili liweze kufanya kazi kisayansi na weledi kama ambavyo viongozi wake wamekuwa wakijinadi mbele ya vyombo vya habari.Tamko hili limetolewa leo Tarehe 08/Desemba/2012.

Joseph Kayinga
Katibu Mkuu-DCPC

USAFIRI WA TRENI WAFUFUKA MWANZA



MAMIA ya wakazi wa jiji la Mwanza, leo walilipuka kwa shangwe na vigelegele wakati wakiilaki treni ya abiria iliyowasili jijini hapo kwa mara ya kwanza baada ya kusitishwa kwa safari zake tangu Disemba 2009. Pichani, treni hiyo ikiwasili leo. Habari za Kina kuhusu ujio wa treni hii Ingia kwenye Ukurasa wetu wa Biashara na Uchumi au BOFYA HAPA

MAHAFALI YA KWANZA SAUTI MTWARA

Saturday, December 8, 2012

 Baadhi ya wahitimu 1147 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara ambacho ni kishiriki cha Saint Augustine (SAUT) wakivishwa Shahada zao katika mahafali yaliyofanyika humo hivi.Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri aw Kazi na Ajira Dr Makongoro Mahanga.
 Baadhi ya wahitimu 1147 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara ambacho ni kishiriki cha Saint Augustine (SAUT) wakivishwa Shahada zao katika mahafali yaliyofanyika humo hivi.Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri aw Kazi na Ajira Dr Makongoro Mahanga.
 Baadhi ya wahitimu 1147 wa Chuo Kikuu cha Stella Maris Mtwara ambacho ni kishiriki cha Saint Augustine (SAUT) wakivishwa Shahada zao katika mahafali yaliyofanyika humo hivi.Mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri aw Kazi na Ajira Dr Makongoro Mahanga.
 Naibu Waziri Waziri wa Kazi na Ajira Dr Makongoro Mahanga akihutubia katika mahafali ya kwanza ya SAUT Mtwara yaliyofanyika Wiki hii mjini humo
 Wanataaluma wa SAUT wakiwa katika maandamano mara Baadhi ya mahafali
 Naibu Waziri akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu aw SAUT Mtwara Askofu Norbert Mtega katika maandamano Mara Banda ya mahafali
 Baadhi ya wazazi na walezi wakiwapongeza jamaa zao kwa kufuzu digrii zao SAUT Mtwara, pichani Benjamin Thompson akimpongeza mdogo wake Sikitu Jackob
 Mara baada ya sherehe hizo wahitimu na jamaa zao walijiandalia sherehe ndogo ndogo Kama hizi hapa katika kumbi hoteli mbalia mbali mjini hum (Picha zote kwa hisani ya Mdau Thompson)

WANACHAMA CHADEMA WAMSHUKIA DK. SLAA

Friday, December 7, 2012


* Ni kwa kukiri kumiliki kadi ya uanachama ya CCM
* Wadai ni mamluki aliyeko Chadema kimaslahi zaidi
* Wamtaka Mbowe, Mkutano Mkuu wamwadabishe.
Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Edo akizungumza leo
DAR ES SALAAM, TANZANIA
ZIKIWA ni siku chache baada ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kukiri kuwa bado anamiliki kadi ya uanachama ya CCM, baadhi ya wanachama wa Chama chake wamemjia juu na kumtaka ajiuzulu nyadhifa zake zote mara moja ndani ya chama hicho.

Aidha wanachama hao wamemtaka Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama hicho Taifa, kumchukulia hatua za kumwadabisha  ikiwemo kumsimamisha, kwa kile walichokiita kuwa ni kadhia mbaya na undumilakuwili alioonyesha kwa kumiliki kadi za vyama viwili vya siasa.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema,  Edo Mwamalala , alipozunfumza na waandishi wa habari leo, katika hoteli ya MIC, Ubungo mjini Dar es Salaam.

"Hatua ya Dk. Slaa kukiri tena bila woga wala aibu kwamba anamiliki kadi ya CCM, inamaanisha kwamba ni mwanachama wa vyama viwili vya siasa yaani CCM na Chadema, kwa tafsiri rahisi ni mamluki hai wa CCM ndani ya Chadema", alisema, Mwamalala ambaye amewahi pia kuwa mgombea wa Ubunge wa Chadema jimbo la Kyela katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mwamalala ambaye alidai kuna wanachama wengi nyuma yake katika kutoa tamko hilo, alidai Dk. Slaa ni kama askari  wa kukodi ndani ya Jeshi la ukombozi, ndiyo maana amedai kulipwa mshahara mkubwa wa zaidi ya sh. milioni saba kwa mwezi kuwauzia Chadema gharama za ukumbozi.

"Itakumbukwa kwamba katika miaka ya tisini  kulikuwa na viongozi machachari ndani ya upinzani wenye maneno ya kuwaaminisha wananchi, huku wakijitutumua kwamba wamekuja kuleta mabadiliko katika nchi hii, kumbe walikuwa mapandikizi waliokuja kuwaacha Watanzania njia panda, sasa Dk. Slaa ni mfano wa hawa", alisema Mwamalala.

Alisema, kwa kukiri kuwa na kadi ya Chama kingine zaidi ya Chadema,  Dk. Slaa amepoteza sifa ya kuwa mwanachama halali wa Chadema kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho, Sura ya Tano, ibara ya tano, kifungu cha kwanza, kipengele kidogo cha nne.

Alisema, mbali na Katiba,  kwa hilo, Dk. Slaa amedhigirisha kuwa hana uadilifu  wala huruma kwa Watanzania walioweka rehani maisha yao kumuunga mkono katika harakati mbalimbali, kiasi cha baadhi ya vijana kuwa tayari kufukuzwa vyuoni wakitetea sera za Chadema.

" Tunawaomba Watanzania wote  wanaounga mkono Chadema, tuungane kwa pamoja kama kweli tunadhamiria kushika dola 2015, watu ndumilakuwili kama Peter Slaa (Dk. Willibrod Slaa) hawatufai tena hata kidogo", alidai Mwamalala na kuongeza;

"Watu kama Peter Slaa( Dk. Slaa), wapo kwa ajili ya kutumia shida za wananchi kujipatia umaarufu huku wakiendesha maisha yao na kuwaacha wananchi wakiteseka".

Mwamalala alidai kwa vyovyote Dk. Slaa bado ni mwanachama wa CCM, awe hai au mfu, kwa sababu hawezi kuikimbia CCM na kuhamia Chadema kwa uchungu mkubwa kama anavyodai, lakini akaendelea kuhifadhi kadi ya chama kisichomfaa tena.

"Ukihama nyumba ya kupanga huwezi kuhama na ufunguo wa akiba, vitu vikipotea kwa mpangaji mpya watajua ni wewe", alisema, na kufafanua kuwa, Kama ni kweli Dk. Slaa amekwisha hama CCM hana sababu ya kubaki na kadi ya chama hicho isipokuwa tu kama bado ana maslahi nacho.

Mwamalala licha ya kuwa bado ni mwanachama wa Chadema ambaye ni Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa, ni miongoni mwa viongozi waliosimamishwa uongozi na Dk. Slaa hivi karibuni kwa madai kuwa ni mamluki wa CCM ndani ya Chadema, ambapo alikuwa Katibu wa Chadema mkoa wa Mbeya.

INTERNATIONAL VOLUNTEER DAY


Dar es Salaam 7 December 2012
Tanzania will on 8 December 2012 celebrate International Volunteer Day (IVD) through a forum on 'Volunteerism and Youth Engagement'  that will be held at Karimjee Hall.The forums is organised by the UN together with Government, Volunteer Involving Organisations, Academia and Youth Groups.

The forum aims to engage youths on volunteerism and encourage them to play their part on volunteerism. Participants includes youths from Universities and out of schools. This year's theme for the Day is :Volunteer Action Counts

IVD is celebrated each year on 5th December.  The Day  was designated by the United Nations in 1985 as an international observance day to celebrate the power and potential of volunteerism. It is an opportunity for volunteers, and volunteer organizations to raise awareness of, and gain recognition for, the contribution they make to their communities.

The act of volunteering is found in all cultures, languages, and religions.  Every year, hundreds of millions of people volunteer their time and skills to help make the world a better place. When they volunteer, they help to improve the lives of others.  And when they volunteer, they also gain a greater sense of belonging to their communities.

On December 5th, people around the world celebrated IVD with rallies, parades, volunteer fairs, group clean ups, blood donations, conferences, exhibitions, fundraising workshops and volunteer recognition events.

The United Nations Volunteers (UNV) programme has been supporting IVD since its inception.  UNV believes that IVD is an ideal opportunity to recognize the significant impact that volunteerism makes worldwide.  IVD enables grassroots voluntary movements to connect with local communities, United Nations (UN) efforts and government authorities.  It is a chance to raise awareness of the contribution volunteers give to the well-being of their community.  Currently, there are approximately 7,300 national and international UN Volunteers contributing to UN work in sustainable development and peace work in over 130 countries.  Below, is the UN Secretary General, Ban Ki-Moons statement to mark the day;

“As we celebrate the impact of volunteers on our world, let us remember the many places they are needed: in war zones and classrooms, in hospitals and homes – wherever struggling people seek a helping hand.

Let us also remember that volunteering can embrace all people, from the activist who works full-time for a cause to the occasional citizen who reaches out when he or she can.  Each sets an example of the spirit of compassion we need.  Each makes a valuable contribution to reaching our common goals.

The timeless act of volunteering in the service of others has taken on new dimensions in today’s digital age.  Anyone with an Internet connection or a mobile phone can make a difference.

I applaud all people who volunteer each year for the benefit of their communities.  I am especially grateful to the 7,700 United Nations Volunteers who support efforts to prevent conflicts, help societies recover from fighting, promote sustainable development, assist in crisis situations and carry out numerous other projects for the greater good.  Their work has advanced the Millennium Development Goals, and I am confident they will also contribute to the progress on the post-2015 development agenda.

Founded on the values of solidarity and mutual trust, volunteerism transcends all cultural, linguistic and geographic boundaries.  By giving their time and skills without expectation of material reward, volunteers themselves are uplifted by a singular sense of purpose.

On this Day, let us renew our determination to offer strength and inspiration to others through volunteerism.”

About UNV: 
The United Nations Volunteers (UNV) programme contributes to peace and development through volunteerism.  UNV is inspired by the conviction that volunteerism can transform the pace and nature of development.  With partners, UNV advocates for volunteerism, integrates volunteerism into development planning and mobilizes volunteers.  The enormous potential of volunteerism is an inspiration to UNV and to volunteers around the world.

Every year, about 7,300 qualified and experienced women and men of around 160 nationalities serve as UN Volunteers in some 130 countries.  They are professionals who play key roles contributing to peace and making an impact on development results.  Annually, there are more than 16,000 online volunteering assignments offered by development organizations through the UNV Online Volunteering service.
For more information.CLICK HERE

Contact info: Ms. Stella Karegyesa, UNV Programme Officer: Tel: +255784338711. Email: stella.karegyesa@undp.org

SIKU 14 ZA KUIONA TANZANIA, MTANZANIA TEMBELEA TANZANIA


DAR ES SALAAM, TANZANIA
Kampuni ya Lakeland Africa ya jiji Dar es Salaam imeandaa safari ya kutembelea hifadhi za taifa na makumbusho ya taifa ili kutoa fursa kwa Watanzania kusherehekea msimu huu wa Krismas na Mwaka mpya.
Watanzania wanahamasishwa  kujitokeza kushiriki katika safari hiyo ya kitalii ya siku 14 itakayoanza jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu hadi Desemba 27 mwaka huu. “Kwako mtanzania sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si lazima kuwa mzungu kuwa mtalii wa ndani”
Safari hii itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani, Lushoto, Tarangire, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Safari hii itatumia magari ya kisasa makubwa yenye uwezo wa kubebe watalii 24 na kutoa nafasi kutumia vifaa vya umeme (laptop, simu, kamera) kwa kila mtalii kuwa na soketi yake. Magari ambayo yamekuwa yakitumiwa na makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa kutumika Tanzania pia.
Gharama za safari hii zinajumuisha chakula, malazi, usafiri, tozo za kuingia hifadhini na tiketi ya ndege kutoka Mwanza kurudi Nyumbani.
Kwa mawasiliano na Lakeland Africa
+255222-761811
+255784885902
Email: reservations@lakelandafrica.com
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’

TANZIA

Tuesday, December 4, 2012


FAMILIA YA MAMA ELIPINA MLAKI INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MAMA YAO MPENDWA  BIBI MARIA ELIA KISAMO, KILICHOTOKEA TAREHE 03 DESEMBA, 2012 KATIKA HOSPITALI YA AGHAKHAN .

TARATIBU ZA MAZISHI ZINAFANYIKA BAOBAB VILLAGE MASAKI, DAR ES SALAAM, NYUMBANI KWA BWANA NA BIBI FREDRICK MLAKI.

MAZISHI YATAFANYIKA USANGI, MWANGA KILIMANJARO TAREHE 08 DESEMBA, 2012 JUMAMOSI SAA NANE KAMILI MCHANA.

HABARI ZIWAFIKIE DR. MAKENGA KISAMO AKIWA MBEYA, DANIEL ELIA KISAMO AKIWA USANGI-MWANGA, BWANA. & BIBI MODEST NA ROSE MERO WAKIWA NEWYORK – MAREKANI, VIOLETH NA CLEMENT MBOYA WAKIWA PHILADELPHIA – MAREKANI, FAMILIA YA UKOO WA MTENGE, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA
BWANA LIHIMIDIWE.

AMEN