Thursday, July 26, 2012

KATA YA KWADELO, KONDOA WATEKELEZA KILIMO KWANZA KWA KASI

0 comments
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Alhaji Omari Kariati (wa tatu kushoto) akiwa kwenye trekta na wakulima wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani (kushoto), Gabriel Galahenga, baada ya kuwakabidhi wakulima hao matrekta maane, kwenye Ofisi za Shirika la Uchumi la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)-SUMA JKT, Mwenge jijini Dar es Salaam, leo Julai 26, 2012. Kufuatia walikuma hao kukabidhiwa trekta hizo nne, sasa Kata hiyo ina trekta 20 zilizopatikana kutoka kampuni hiyo kwa udhamini wa diwani Kariati. Trekta moja  ambayo inauzwa kwa sh. milioni 20 wakulima hao wanakabidhiwa kwa kulipa nusu ya bei hiyo na kisha kulipa  zilizobaki katika kipindi cha miaka minne kwa udhamini wa diwani huyo.
 Diwani Kariati akikabidhi funguo ya trekta kwa mmoja wa wakulima  wa Kata hiyo, Abdallah Ramadhani. Wengine ni wakulima wa Kata hiyo, Alifa Hulufya (kulia), Chundu Damiani (wapili kushoto) na Gabriel Halahenga (watatu kushoto) na kati yao ni Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan.
 Diwani Kariati akikabidhiwa barua na mkulima wa Kwadelo,  Gabriel Halahenga, wakati wa hafla ya diwani huyo kukabidhi matrekta maane kwa wakulima wa kijiji hicho leo, Ofisi za Suma KJT, Mwenge, Dar es Salaam.  Wengine ni,  Alifa Hulufya (kulia), Chundu Damiani (wapili kushoto) na Gabriel Halahenga (watatu kushoto) na kati yao ni Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan. Barua hiyo ni kwa ajili ya Dhukurani kwa Mkuu wa JKT kutokana na Suma JKT kukubali kuwapa matrekta wakulima wa Kwadelo, kwa malipo ya nusu ya gharama na kumalizia deni katika kipindi cha miaka minne baadaye.
 Meneja wa Mradi wa zana za Kilimo wa Suma JKT,  Kanali Felix Samillan akifurahia jambo na Diwani Kariati wakati wa makabidhiano ya trekta hizo.
Diwani Kariati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhi trekta nne kwa wakulima wa kata yake leo.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....