Tuesday, July 10, 2012

MATAIFA YATAKA MKATABA WA BIASHARA YA SILAHA ( ATT)USIINGILIE UHURU WA NCHI KUJILINDA

1 comments

Na  Mwandishi Maalum, New York
Mkutano  wa majadiliano kuhusu uanzishwaji wa Mkataba wa Kisheria wa Biashara ya  Silaha Duniani umeingia katika wiki yake ya pili huku kila nchi ikijaribu kutoa msimamo wake  kuhusu mwelekeo wa mkataba huo na nini kiingizwe au kipi  kisiingizwe.
 Kwa ujuma kila nchi imekuwa ikisisitiza kwamba  mkataba huo lazima pamoja na umuhimu wake wote uzingatie uhuru na haki ya nchi kujilinda na kulinda mipaka yake
Baadhi ya nchi zimeweka  wazi misimamo yao  na kusema hazitauridhia mkataba  iwapo  utakuwa na mwelekezo wa kudhibiti au kuathiri sera za nchi kuhusu suala zima la kujilinda  au kuathiri maslahi ya  kiusalama ya nchi husika ikiwamo  kuingilia uhuru na misingi ya nchi kujiamulia mambo yake yenyewe au kuingilia masuala yake ya kisiasa.
 Aidha   mapendekezo ya   wasemaji wengi ambao wamekwisha kuzungumza, wanasisitiza sana uwazi na ukweli katika majadiliano ya mkataba huu, huku wakibainisha  kwamba kwa namna yoyote ile itakavyokuwa mkataba huo usiwe na upendeleo kwa  nchi chache na kuzibana   nchi  nyingi hasa zinazoendelea .
 Ujumbe wa Tanzania katika mkutano  huu  ambao unajikita katika kutoka na mkataba utakao ratibu na kudhibiti biashara ndogo ndogo  na  nyepesi , unawakilishwa na  wataalamu kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania,   Polisi,   Idara ya Mambo ya Nje (Ofisi ya Rais),  na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Wasemaji wengi wamesisitiza haja na umuhimu  wa mkataba huu kuwabana pia watengenezaji wa silaha badala ya kuwabana waagizaji peke yake.
Aidha baadhi ya wasemaji wameeleza wazi kuwa   hawataraji kwamba mkataba huu uzibane tu nchi zinazoagiza silaha bali  uwabane hata   makundi na watu wanaofanya biashara  au kuzisambaza  silaha  kinyume na sheria.
Wachangiaji wengine wamesisitiza haja na umuhimu wa kuhakikisha kwamba mkataba huu utakuwa na vipengele vyenye ushawishi  utakaopelekea nchi nyingi zaidi  kuuridhia mara tu  utakapo andaliwa.
Na Hivyo wamesisitiza kwamba itakuwa jambo  jema  sana kama mkataba huo utaridhiwa na  nchi zote bila ya kupigiwa kura.
 Wazungumzaji  wengine wamesisitiza kwamba  mkataba huu ambao utakuwa wa kisheria  lazima ufafanua  vyema na kwa lugha nyepesi na inayoeleweka  na kuweka wazi madhumuni na malengo halisi ya mkataba huo.
Tanzania   inatarajiwa kuwasilisha msimamo na mchango wake wiki hii  kwa mujibu wa ratiba ya wazungumzaji itakavyopangwa.

1 comments:

Charles Nazi said...

Napenda kuwaarifu kwamba sasa, kitabu cha mbinu za biashara na maarifa ya kupata pesa na utajiri, unaweza kukipata kwenye email yako kwa mfumo wa PDF. Kwa wale wanaohitaji wanaweza kunitumia Sh. 5,000 kwa M PESA kwenye simu namba 0755394701 kisha kunitumia email zao na mimi nitawatumia email iliyoambatanishwa na kitabu.

Kitabu hiki kinalenga kumsaidia mtu yeyote ambaye anatafuta utajiri kwa kufanya biashara ndogondogo hadi kubwa. Pia kinatoa maarifa, mbinu na mikakati mbalimbali ya kupambana na umaskini, kinatoa elimu ya biashara na mbinu mbalimbali za namna ya kupata pesa kwa njia halali ili kukurahisishia safari yako ya kuelekea kwenye kutafuta na kupata utajiri. Kitabu hiki kina sehemu mbili, sehemu ya kwanza inaeleza kuhusu taratibu za kuanzisha biashara sheria, utafiti wa masoko, utunzaji wa hesabu za biashara na utatuzi wa matatizo ya biashara. Sehemu ya pili inaelezea kuhusu mawazo, mbinu mbalimbali za biashara unazoweza kuzifanya na kupata faida na hivyo kutajirika.
CHARLES NAZI
http://www.squidoo.com/kitabu-mbinu-za-biashara

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....