Thursday, July 26, 2012

MELI TATU ZAFUTIWA USAJILI ZANZIBAR

0 comments
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanziba
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar, imezifutia usajili meli tatu za abiria baada ya kuonekana kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa abiria waacha kutoa huduma za usafiri majini ili kuepuka ajali.
    Meli zilizofutwa ni Seagull, MV Kalama ambayo ni nyenzake na Mv Skagit iliyozama baharini wiki iliyopita na MV Sepideh ambazo zote zilikuwa zikifanya safari zake kati ya Zanzibar na Dar es Salaam na Zanzibar na Pemba.
    Uamuzi wa kuzifutia usajili meli hiyo umetangazwa leo na Kaim Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar (ZMA) Bw. Abdullah Hussein.
     Kufuatia uwamuzi huo, Serikali ya Mapinduzi ya Sanzibar, imetoa siku 30 kuanzia leo kwa wamiliki wa Meli hizo wawe wameshaziondoa meli zao kwenye maegesho ya meli Bandarini ili kutoa nafasi ya meli halila kuegeshwa bandarini hapo.
    Hatua hiyo imekuja siku chache tu baada ya kuzama kwa meli ya Skagit na kusababisha vifo vya zaidi ya abiria 100 na wengine 146 kunusurika baada ya kuokolewa na wazamiaji wa vyombo vya ulinzi na usalama, mamlaka ya Bandari na wapoigambizi wa makampunu binafsi.
   Wakati huo huo, hadi wakati natuma taarifa hizi, maiti zilizooolewa zimefiukia 123 baada ya kupatikana kwa maiti nyingine 17 na nyingine tano kupatikana na kuzikwa kwenye fukwe za Pwani ya Bagamoyo mkoani Pwani.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....