Friday, July 27, 2012

MEYA WA JIJI ANG'OLEWA MWANZA

0 comments
MWANZA< TANZANIA,
Meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza, Japheth Manyerere, ameng’olewa kwa madai ya madiwani wa Halmashauri hiyo, kutokuwa na imani naye.
   Manyerere amengh'olewa leo kwenye kikao cha baraza hilo kilichofanyika kwenye ukumbi wa jiji, na kuongozwa na Naibu wake Charles Chinchibea, kabla ya kumvua wadhifa huo kwa kura 20 zilomkataa huku nane zikumuunga mkono.
    Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, kikao hicho kilikuwa maalum kwa jaili kumjadili Manyerere baada ya kuwepo kwa hoja za kutokuwa na imani naye zilizoibuliwa na baadhi ya madiwa ni Chama chake cha CHADEMA katika Kikao cha Baraza mwezi uliopita.
   Kabwe, jana alisema kwamba kwamujibu wa kanuni za Halmashauri, Manyerere si Mkurugenzi tena na hivyo utafanyika mchakato wa kumchagua Meya mwingine miongoni mwa madiwani wa vyama vya CCM, Chadema na CUF wanaounda Halmashauri hiyo.
   “Amepigiwa kura 20 za hapana na kupata kura nane za ndiyo, hiyo inaonekana wazi kwamba Chama chake ambacho ikina  Madiwani wengi kina mchango mkubwa wa kumng’oa.” Alisema Kabwe wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
     Kabla ya Manyerere kuenguliwa kwa kura hizo, chama chake kilimpa siku nne ajiuzulu kwa hiari lakini alikataa na kudai wafanye wanalotaka.
    “Awali siku zilizopita katika kikao cha chama tulimpa siku nne za kujiuzulu kwa hiari lakini hakutekeleza na juzi katika kikao cha Kamati ya Madiwani wa chama pia alikataa kuachia ngazi akidai tufanye tunalotaka.” Alisema Diwani mmoja wa Chama hicho ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa vile si msemaji.
     Katika kikao kilichopita cha baraza hilo, Diwani wa Kata ya Igoma Adam Chagulani ndiye aliyekuwa wa kwanza kuibua hoja ya kutokuwa na imani na Meya huyo kwa madai ya kushindwa kuendesha vikao kikamilifu na kukika kanuni na taratibu za Halmashauri hiyo ikiwa pamoja na kutoa siri za jiji nje (kwa wafanyabiashara)
     Katibu wa Chadema wa mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi alithibitisha chama chake kumng’oa kwa tuhuma mbalimbali 11 ambazo alidai ni pamoja na kushindwa kusimamia maendeleo badala yake kusimamia ujenzi wa Kanisa moja.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....