Saturday, July 21, 2012

NAPE, MAWAZIRI KUFUNIKA KIGOMA JUMAPILI HII

0 comments
KIGOMA, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesho, Jumapili hii, Julai 22, kinatarajiwa kuutikisa mkoa wa Kigoma, kwa mkutano wake mkubwa wa hadhara, utakaofanyika kwenye Viwanja vya Communicy Cetre mjini Mwanga mkoani hapa.
    Mkutano huo mkubwa umepangwa kuhutubiwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye, na baadhi ya mawaziri walioalikwa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM katika sekta wanazohusika nazo.
    Mkutano huo, umepangwa kuanza mapema kwa kuwa unatakiwa kumalizika saa kumi jioni ili kuwapa fursa wananchi waliofunga kwenda kufuturu baada ya kushinda ana swaumu ya Mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
   Awali Mkutano huo ulikuwa ufanyike, Ijumaa iliyopita, lakini ukalazimika kusogezwa mbele baada ya taifa kuingia katika maombolezo ya siku tatu, kufuatia ajali ya meli iliyotokea Zanzibar ambapo watuzaidi ya 50 wamefariki dunia.
  Katika mkutano huo wa kesho Jumapili, Nape na baadhi ya mawaziri na manaibu mawaziri walioalikwa akiwemo Steven Wasira na Aggrey Manri,  wanatarajiwa kueleza utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Kigoma na Tanzania kwa jumla.
  Pia wanatarajiwa kueleza sera za CCM, na kueleza wananchi wa Kigoma, nini CCM imefanya, inafanya sasa na inatarajiwa kufanya nini baadaye katika kukifanya chama hicho na serikali yake, kuendelea kuwa makini na imara katika kuliongoza taifa la Tanzania.
   Kufuatia mkutano huo kuahihirishwa  karibu kona zote za mji wa Kigoma na vitongoji vyake kama Ujiji, Kahabwa, Gungu na Mwandiga, wamekuwa wakijadili kuhusu mkutano huo, kwenye vijiwe vya kahawa, vituo vyua daladala na kwenye mikusanyiko hasa ya vijana, hamu kubwa ikiwa ni kutaka kumsikiliza Nape na wabunge watakaopanda jukwaani kwa mtindo wa aina yake.
   Pia baadhi ya watu wameonyesha hamu ya kuhudhuria mkutano huo kutokana na staili ambayo inaelezwa kuwa ni mpya na nzuri ya CCM kuwapeleka kwenye mikutano ya hadhara baadhi ya mawaziri kueleza wanavyosimamia utekelezaji wa ilani ya Chama kwenye sekta zao.
   "Kwanza mimi ningependa nimsikie Nape, nasikia ni msema kweli kama kuna jambo huwa hasiti kusema hata kujwaani, na pia nitapenda niwasikie mawaziri watakaowaleta kwa sababu kwa muda mrefu hatujawahi kumsikia hapa Kigoma waziri yeyote akisimama jukwaani kwenye mkutano wa hadhara kueleza utekelezaji wa ilani", alisema Joseph Chishako wa Mwandiga.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....