Thursday, July 26, 2012

RAIS KIKWETE AKIKUTANA NA ASKOFU MKUU RUGAMBWA, IKULU

0 comments
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na kufanya mazungumzo na Askofu Mkuu Protase Rugambwa ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedict wa XVI kuwa Katibu Mwambata wa Idara au Kongregasio ya Uenezaji wa Injili kwa ajili ya Mataifa na Rais wa Mashirika ya Kipapa ya Kimisionari yenye makao yake, Roma. Wakati wa mazungumzo hayo Rais Kikwete kwa mara nyingine tena,amempongeza Askofu Rugambwa kwa uteuzi wake na kusema kuwa uteuzi huo ni kielelezo dhahiri cha imani kubwa aliyonayo Baba Mtakatifu kwa askofu huyo na kuwa ni heshima kubwa kwa Mtanzania kupata nafasi ya kushika wadhifa huo mkubwa. Kabla ya Uteuzi huo Askofu mkuu Rugambwa alikuwa askofu wa jimbo Katoliki Kigoma. Pichani, Rais Kikwete akiagana na Askofu Mkuu Rugambwa bada ya mazungumzo yao.(Picha na Freddy Maro)

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....