Monday, July 16, 2012

WABUNGE VIJANA KUPIGA KWATA JKT

0 comments
DODOMA, TANZANIA
Wabunge vijana wote wataanza mafunzo  maalumu ya Jeshi la Kujenga Taifa, kuanzia Machi 2013, kwa lengo la kuwajengea uzalendo.
     Pia, serikali imetengaza rasmi kwa mujibu wa sheria kuanza kwa mafunzo ya jeshi la kujenga taifa kwa vijana nchini yatakayoanza mwakani na watakaohitimu  kidato cha sita 2013 watakuwa miongoni mwa watakaoanza.
    Akisoma  makadirio ya  Mapato na Matumizi  kwa mwaka 2012/2013, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha (Pichani),  Bungeni, Dodoma, leo , alisema kwamba mafunzo hayo yataanza kwa mujibu wa sheria.
     Nahodha alisema kwamba katika bajeti ya bunge ya mwaka 2011/2012, alipokea ombi la wabunge vijana kuandaliwa mafunzo maalumu ya jeshi la kujenga taifa, hivyo serikali imelikubali ombo hilo .
       “Nafurahi kuliarifu bunge lako tukufu kwamba wizara yangu imelifanyia kazi ombi hilo na kuandaa utaratibu wa mafunzo maalumu ya wiki tatu kwa waheshimiwa wabunge vijana,”alieleza.
      Alisema kwamba  mafunzo hayo yataanza Machi, 2013 sanjari na kuanza rasmi kwa mafunzo ya vijana kwa mujibu wa sheria.
      “Kwa hiyo waheshimiwa wabunge vijana wataungana na kundi la kwanza la vijana 5,000 watakaoanza mafunzo hayo.ni imani yetu waheshimiwa wabunge kunufaika na mafunzo hayo, watahamaisha zoezi la urejeshwaji wa mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria na kutoa taswira nzuri ya mafunzo haya kwa jamii,”alieleza nahodha. Pia, aliwataka wabunge vijana waanze kujiorodhesha kwa ajili ya mafunzo  hayo.
      Nahodha alieleza kwamba maandazili ya kuanza kwa zoezi hilo yamekamilika ambapo JKT wako tayari kuchukua vijana 20,000 kwa wakati mmoja ingawa  alieleza kwamba gharama za kuendesha mafunzo hayo ni kubwa.
      Kutokana na ukubwa gharama kutoa mafunzo kwa vijana wote hao, wizara hiyop  haitaweza kuchukua vijana wote wanaostahili kupitia JKT kwa mujibu wa sheria na badala yake watachukuliwa vijana 5,000 kwa kuanzia.
     “Kutokana na hali ya hiyo serikali inapanga kurejesha  mafunzo hayo ya majaribio kwa vijana 5,000. Vijana hao ni miongoni mwa vijana 41,348 ambao watahitimu mafunzo ya kidato cha sita mwaka 2013,”alieleza.
      Alisema kwamba kuwa kuwa kupata vijana 5,000 ni kazi kubwa, wizara imeweka vigezo maalumu vya kuwapata  kwa kuzingatia makundi  ambayo yatatangazwa Januari, mwakani.
       Kwa mujibu wa Waziri Nahodha, mafunzo hayo  yatakayoanza machi mwakani,  yatakuwa ya miezi sita katika kambi za Bulombora na Kanembwa (Kigoma), Mlale (Ruvuma) Mafinga (Iringa), Msange (Tabora),na Oljoro (Arusha).

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....