Sunday, August 5, 2012

AIRTEL YAFUTURISHA WATEJA WAKE ARUSHA

0 comments
ARUSHA, TANZANIA

Wakati jamii ya waislamu wakiwa katika mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeandaa futari kwa ajili ya wateja wao wakubwa walipo katika makampuni mbalimbali mkoani Arusha.

Akizungumzia hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Naura Springs jijini Arusha meneja utoaji huduma wa Airtel Hilda Nakajumo amesema kampuni hiyo kwa kutambua umuhimu wa mfungo wa mwezi mtukufu wa
ramadhani inaungana na waislamu kwa kuandaa futari kwa wateja wao mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii.

 " Tunawaunga mkono sana ndugu zetu waislam katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan na ndio maana tuko wote katika kufuturu ili kuonyesha umoja na kuunga kwetu nao. Tunaomba wale wote wanofunga kweli basi na wasikate tamaa mpaka mwisho kama mafundisho yanavyofundisha", alisema Hilda.

Kwa upande wao baadhi ya wateja waliopata fursa ya kushiriki katika futari hiyo wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kutambua umuhimu wa mwezi huo kwa kuwakumbuka waumini  wa dini ya
kiislamu.

Kipindi hiki Waislamu kote nchini wanaungana na waislamu wengine duniani kutekeleza nguzo ya nne kati ya tano katika uislamu.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....