Wednesday, August 1, 2012

ASILIMIA 21 YA UCHUMI WA AFRIKA UNAYUMBISHWA NA WATAALAM WA KUGUSHI

0 comments
NA ROSE JACKSON, ARUSHA ,TANZANIA
IMEBAINIKA kuwa asilimia 21 ya uchumi wa nchi za Afrika Mashariki kwa kila mwaka  unayumbishwa na ughushi wa aina mbali mbali ukiwemo wa luku za umeme ,fedha pamoja na kodi hali ambayo inachangia kiwango kikubwa cha umasikini
     Hayo yameelezwa na Sosthenes Bichanga ambaye ni Mwakilishi  wa Shirika la Kimataifa la kupambana na ughushi na biashara ya fedha haramu la Ossulivan Association Kenya, wakati akiongea na waandishi wa habari mapema jana jijini hapa.
    Alisema kuwa kiwango hicho cha fedha ambazo zinapotea kwa kila mwaka kinasababishwa na sababu mbalimnbali ndani ya nchi hizo za Afrika ya Masharikii mara baada ya kufanyika utafiti wa siri katika maeneo ya nchi hizo, ambapo kwa sasa wamejipnga kuhakikisha kuwa wanatoa elimu zaidi hasa elimu ya Kiuasibu ili kukwepa hasara hizo.
     Pia alisema kuwa zoezi hilo la kugushi fedha hasa kwenye  Taasisi za Fedha pia zinatokana na elimu finyu ambayo wananchi wanayo hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa wakaguzi na wahasibu kupatiwa mbinu mbali mbali za kuthibiti hali hiyo
    “Tafiti zilizofanyika zinaonyesha mamlaka mbali mbali za mapato ya nchi za afrika yanavamiwa na wataalamu wa kughushi na hatimaye wanajikuta wanaletewa nyaraka zinazoonyesha kuwa kodi imelipwa na wanapotazama mfumo wa ndani wa mawasiliano malipo yanakuwa hayajaingia huu ndio ughushi tunaotaka kuuthibiti kwa wale wanaofanya hivyo”alisema Bichang”a
   Aliongeza kuwa hali hii ya juu ya kiugushi wa kieletroniki  imesababisha hasara kubwa ndio maana makampuni mengine ya umeme hayajitoshelezi kwani yanajipanga kupata faida na mwisho wa siku yanaishia kupata hasara
     Kutokana na hali hiyo ya ughushi shirika hilo limeandaa kongamano litakalofanyika wiki ijayo mjini hapa  kwa ajili ya kutoa  mbinu za kiuasibu za kuchunga na kukagua fedha, ambapo watu elfu nne watahudhuria wakiwemo maafisa wa tra,maafisa wa benki,maafisa ugavi wa umeme,wahasibu,maafisa wa takukuru,wakaguzi wa mahesabu pamoja na wakurugenzi wa mashirika.
      Awali mwakilishi wa kongamano hilo kwa mjini hapa Solomon Njiamoja alisema kuwa wahasibu na wakaguzi wanapaswa kutumia fursa hiyo ya kujifunza mbinu mbali mbali za kupambana na ughushi ili waweze  kuthibiti wizi unaotokea mara kwa mara

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....