Wednesday, August 29, 2012

CRDB BANK KUMEKUCHA TABATA, TAWI LAKE JIPYA LAHUDUMIA WASTANI WA WATEJA 300 KWA SIKU

0 comments

 DAR ES SALAAM, TANZANIA
BENKI ya CRDB, imezidi kutekeleza lengo wa kufikisha huduma zake kwa Watanzania wengi zaidi na sasa imefungua tawi jipya eneo la Tabata Magengeni,wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, na kuwa benki pekee yenye tawi katika eneo hilo.

Tawi hilo limeshaanza kufanyakazi tangu Julai 2 mwaka huu, ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa Wakazi wa Tabata na maeneo ya jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa tawi hilo, Hawa Sasya alisema wateja wa Tabata na maeneo ya jirani sasa wanaweza kupata huduma za kibenki  katika tawi hilo.

Alisema, tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa ni mkombozi kwa wateja mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo na hata taasisi za kiroho kama misikiti na makanisa.

“Tawi lipo karibu na Kanisa la Kristo Mfalme, Tabata Magengeni, ambapo linatoa huduma mbalimbali zikiwemo za; Mashine ya kutoa na kuweka fedha (ATM) ambayo hufanyakazi kwa muda wa saa 24”alisema

Alitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na Tembo Card Visa, Akaunti ya Hundi na ya watoto inayojulikana kama Junior Account pamoja na Akaunti ya Akiba.

Hata hivyo aliongeza kuwa, tawi hilo litakuwa likitoa Akaunti ya Tanzanite, na huduma za mikopo mbalimbali na huduma za bima.

Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi limekuwa likitoa pia huduma ya kibenki kwa kutumia Simu ya mkononi (SimBanking), pamoja na Akaunti ya Wanafunzi ambayo inafahamika kama Scholar Account.

Meneja huyo aliwataka Wananchi na wateja wapya kutumia tawi hilo ili kupata huduma za kibenki badala ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyombali

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....