Wednesday, August 22, 2012

DC SERENGETI AFARIKI DUNIA

0 comments

MKUU wa wilaya ya Serengeti Kepteni Mstaafu, James Lyamungu amefariki dunia katika hospitali ya Taifa  Mhimbili, Dar es Salaam, alikokuwa amehamishiwa ili kupata matibabu ya kina.

Awali Mkuu huyo aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuhamishiwa katika hospitali ya mhimbili baada ya hali yakekuzidi kubadilika.

Marehemu Lyamungu amefariki dunia leo asubuhi  wakati akipewa matibabu katika hospitali  hiyo ya mhimbili na mwili wake umehifadhiwa .

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mara John Tuppa amesema  kuwa taarifa za msiba  wa mkuu aliyekuwa  mkuu wa wilaya ya Serengeti amezipokea na kwamba wasemaji wakuu juu ya msiba huo ni Makao Makuu.

“Taarifa za Kifo cha marehemu tumeishazituma makao makuu sisi kama mkoa sio wasemaji kwani sio kila mtu atoe taarfa hizi tusubiri zitatolewa na makao makuu kwa vyombo vya habari”,alisema Tuppa.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....