Thursday, August 30, 2012

KATIBU MKUU WA CCM YUPO AFRIKA KUSINI

0 comments
CAPTOWN, AFRIKA KUSINI 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama, yupo Afrika Kusini kuhudhuria Mkutano wa 24 wa Socialist International unaofanyika katika Jiji la Capetown.
Mkutano wa 23 ulifanyika Athens, Ugiriki mwaka 2008.

Mkutano huo ambao ni wa kwanza kufanyka Afrika unaoanza Agosti 31 hadi Septemba 2 mwaka huu utahudhuriwa na vyama wanachama vipatavyo 150 kutoka nchi mbalimbali duniani. Hata hivyo, CCM inahudhuria mkutano kwa kualikwa kama mtazamaji tu, kwani si mwanachama wa Socialist International.

Katika mkutano huo uliobeba ujumbe unaosema " For a New Internationalism and a New Culture of Solidarity", pamoja na mambo mengine, pia watafanya Uchaguzi kumpata Rais, Makamu wa Rais na Katibu Mkuu. Rais wa sasa wa umoja huu ni aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Ugiriki, George Papandreou na Katibu Mkuu wake ni Luis Ayala raia wa Chile.

Waliowahi kuwa marais wa Socialist International tangu ilipoanzishwa mwaka 1951, ni Morgan Phillips
(Uingereza), Alsing Andersen (Denmark), Erich Ollenhauer (Ujerumani Magharibi), Bruno Pittermann (Austria), Willy Brandt (Ujerumani Magharibi), Pierre Mauroy (Ufaransa), Antonio Guterres (Ureno),
na wa sasa Papandreou wa Ugiriki.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu ni Julius Braunthal (Austria), Bjarne Bratoy (Norway), Albert Carthy (Uingereza), Hans Janitschek (Austria), Bernt Carlsson (Sweden), Pentti Vaananen (Finland) na wa sasa Ayala kutoka Chile.

Socialist International ilianzishwa mwaka 1951 ikichukua nafasi umoja uliojulikana kama Labour and Socialist Inernational wanachama wake wakiwa ni vyama kutoka Ulaya ya Magharibi tu. Hivi sasa kuna vyama 15 kutoka katika nchi 14 ambavyo ni wanachama wa kudumu wa Socialist International katika bara la Afrika.

Nchi zenye vyama wanachama katika Afrika ni Benin (MIR), Cameroon (SDF), Cape Verde (PAICV), Equatorial Guinnea (CPDS), Ghana (NDC), Guinnea (RPG), Mali (ADEMA-PASJ na RPM), Mauritania (MMM), Msumbiji (FRELIMO) Namibia (SWAPO), Afrika Kusini (ANC), Senegal  (PS) na Zimbabwe (MDC). 

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....