Sunday, August 5, 2012

MIAKA THELATHINI JELA KWA KULAWITI KAVULANA KA MIAKA 12, KIBAHA

0 comments
NA JOHN GAGARINI, KIBAHA, TANZANIA
MKAZI wa Umelani wilayani Kibaha mkoani Pwani Bw Omary Ally (31) amehukumiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana mwenye umri wa mika (12) ambaye ni mpwa wake.

Hukumu hiyo ilitolewa na hakimu mkazi  mwandamizi wa mahakama ya wilaya Kibaha Bi Salome Mshasha chini ya mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi Insekta Kulwa Merdad alisema kuwa mshitakiwa  alialitenda kosa hilo Januari 18 mwaka huu majira ya saa 6 usiku huko mtaa wa Umerani.

Mahakama ilielezwa kuwa wakati mtuhumiwa alitenda kosa hilo mkewe alikuwa kwao akisubiri siku za kujifungua na alipokwenda kumsalimia mkewe nyumbani kwao alikuta amekwenda hospitali na kukaribishwa na wenyeji wake alale na wapwa zake wawili na ndipo alipomlawiti mtoto huyo.

Kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo mwendasha mashitaka alitaka mtuhumiwa apewe adhabu kali kutokana na tukio hilo ili iwe fundisho kwake na jamii kwani kitendo hicho ni cha kinyama na mshitakiwa hastahili kukaa na jamii iliyostaarabika.

Akijitetea mahakamani hapo mshtakiwa aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwani yeye ni mgonjwa na anatumia dozi halafu ni baba wa familia ya mke na wawtoto wawili wanaomtegemea.

Hakimu Mshasha akitoa adhabu hiyo alisema kuwa mshitakiwa alikuwa na dhamana ya kulinda haki za mtoto huyo na si kuzivunja kama alivyofanya jambo ambalo ni unyanyasaji na udhalilishaji mkubwa na kuwa adhabu ya makosa kama hayo inajulikana.

Alisema baada ya kupitia ushahidi na vilelezo vilivyotolewa na upande wa mashitaka amejiridhisha na kutoa adhabu hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia yaka hiyo.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....