Monday, August 20, 2012

MREMBO LISA JENSEN AREJEA NYUMBANI

0 comments

Mrembo Lisa Jensen ambaye ni Miss World Tanzania 2012 amerejea jijini Dar es Salaam leo akitokea nchini China alipokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia mwaka huu na kupokelewa na viongozi kadhaa wa Kamati ya Miss Tanzania akiwepo Mkurugenzi wa Kino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania Hashim Lundenga (kulia) aliyefika uwanja wa ndege wa JNIA Dar es salaam kumpokea.
Lisa akizungumza na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, kutoka kushoto, Katibu Mkuu, Bosco Majaliwa, Mrembo Amisa Hassan, Mkurugenzi Hashim Lundenga na Ofisa Habari wa Kamati, Haidan Rico
Lisa akila pozi ya picha na mmoja wa warembo waliofika kumpokea Amisa Hassan. Lisa alifanikiwa kuingia Robo fainali za Top Model na kumi na kumi bora ya Shindano la Multmedia Award 2012. SOURCE:www.mrokim.blogspot.com 

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....