Saturday, August 18, 2012

MWANDISHI WA HABARI MWANDAMIZI AFARIKI DUNIA

0 comments

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Ofisa Mwandamizi  wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Alfred Mbogora, amefariki dunia.
  Taarifa zilizotufika katika mtandao wa Daily Nkoromo Blog na Tanzania Vision Blog, zinasema kwamba, Mbogora amefariki dunia leo Agosti 18, 2012, katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam,  alikokuwa amelazwa baada ya kuugua ghafla.
  "Siku ya jumatano wiki hii, aliuguwa ghafla akiwa safarini kwenda Bagamoyo kikazi, akiwa  njiani akasema anajisikia vibaya kisha akapoteza nguvu.
   Alfred Mbogora (pichani) amefanyakazi za uandishi wa habari kwa siku nyingi, tangu lililokuwa Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA) Magazeti ya The Guardian na The African na kufanya kazi pia katika taasisi ya Utafiti na Demokrasia(REDET). Mtayarishaji Mkuu wa Blogu za Nkoromo Daily na Tanzania Vision, Bashir Nkoromo kwa niaba ya na timu yote ya waandaaji wa blogu hizi anatumia fursa hii kutoa pole ya dhati kwa ndugu jamaa na marafiki hasa jamii ya waandishi wa habari kwa jumla kutokana na kuondokewa na 'jembe' mwenzetu.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....