Wednesday, August 1, 2012

RAIS KIKWETE AMTEUA MSAIDIZI WAKE KITENGO CHA UCHUMI MASUALA YA ELIMU

1 comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bibi Karolina Albert Mthapula kuwa Msaidizi wa Rais – Kitengo cha Uchumi (Masuala ya Elimu).
Taarifa iliyotolewa leo, Jumatano, Agosti Mosi, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Y. Sefue kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais – Ikulu, inasema kuwa uteuzi huo unaanza leo hii.
Kabla ya kuteuliwa kwake, Bibi Mthapula alikuwa Ofisa Elimu katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

1 comments:

emu-three said...

Tupo pamoja mkuu ,shukurani kwa kuwa ukitupa habari hizi tupo pamoja

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....