Saturday, August 4, 2012

UMOJA WA MATAIFA WAJARIBU TENA KUIBANA SYRIA

0 comments
Ubao ukionyesha namna  kila nchi ilivyopiga kura wakati   Baraza  Kuu la  Umoja wa Mataifa, lilipokutana siku ya Ijumaa kulipigia kura Azimio liliwasilishwa na Saudi Arabia. Azimio   ambalo pamoja  na mambo mengine lilikuwa linajaribu kutoa shinikizo  kwa utawala wa Syria kuacha matumizi ya silaha dhidi ya wananchi wake, lakini wakati huo huo Azimio hilo  kutoonyesha  ukali wowote kwa  upande wa Upinzani, vikundi vya kigaidi au nchi ambazo zimekuwa zikiwapatia wapinzani silaha. Azimio hili limepitishwa kwa kupigiwa kura ambapo nchi 133 zimeunga mkono, 12 zimepiga kura ya hapana huku 31 zikipiga kura ya kutofungamana na upande wowote.  nchi ambazo zimepiga kura ya hapana na zile ambazo  hazikufungamana na upande wowote baadhi zimeeleza kwamba zimechukua hatua hiyo kutokana na ukweli kwamba azimio hilo  limeegemea zaidi upande mmoja, lakini pia lilikuwa linaingilia masuala  ya ndani ya nchi huru jambo  ambalo ni kinyume na  sheria za kimataifa

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....