Saturday, August 18, 2012

MWENGE WA UHURU WAPATA AJALI BUNDA, 15 WANUSURIKA

0 comments

BUNDA, TANZANIA
ZAIDI ya watu 15 wakiwemo waandishi wa habari, jana wamenusurika kifo, baada ya magari matatu yaliyokuwa kwenye msafara wa mwenge wa uhuru kugongana wilayani Bunda, mkoani Mara.

Katika tukio hilo magari mawili yameharibika vibaya, likiwemo la taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) walilokuwa wamepanda pia waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari, akiwemo mwandisi wa habari hizi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi, ambapo gari moja mali ya halmasauri ya wilaya lenye namba za usajili SM 8809, iligonga kwa nyuma gari ya TAKUKURU yenye namba za usajili T. 645 BCT.

Hali hiyo ilisababisha magari mengine kugongana na kuaacha njia likiwemo la TRA lenye namba za usajili STJ 9663, ambapo pia kama zisingekuwa juhudi za madereva wa magari mengine kufanya jitihada za makusudi kwa kuacha barabara na kuingia upande mwingine uhenda ingekuwa ajali kubwa sana.

Katika tukio hilo kakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa, ambapo baadhi yao wamepata maumivu ya kawaida tu.

Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa ajili hiyo iliyotokea majira ya jioni katika kijiji cha Kasahunga, kwenye barabara kuu ya Bunda-Ukerewe, wakati msafara wa mwenge huo ukielekea kwenye mkesha katika kijiji cha Kibara, baada ya kuzindua na kuweka mawe ya misingi kwenye  miradi 9 ya maendeleo iliyogarimu zaidi ya sh. bilioni 1.4. 

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....