Monday, September 17, 2012

KITUO CHA AFYA KWADELO CHAKUMBWA NA UHABA WA WATUMISHI

0 comments

Na Dotto Mwaibale, Aliyekuwa Kondoa
KITUO cha Afya cha Kata ya Kwadelo kilichopo katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa wafanyakazi hali inayoleta usumbufu kwa wananchi wa Kata hiyo ya kwenda Hospitali ya Wilaya hiyo kupata matibabu.

Akikuzngumza na waandishi wa habari katika Kata hiyo Muuguzi Mkuu wa Kituo hicho Salma Belindani alisema mahitaji halisi ya wahudumu wa kituo hicho ni 12 lakini hivi sasa wapo wawili hali inayowafanya kuwa katika mazingira magumu ya utendaji kazi.

Alisema kuhusu tatizo hilo tayari wamewasiliana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hivyo huenda wakati wowote wamaweza kupata watumishi wengine kwa siku za mbeleni.

Alisema kituo hicho kilikuwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kukosekana kwa taa hivyo kuleta adha kwa wagonjwa na waja waxzito waliokuwa wakifika kupata huduma  akini kwa hivi sasa Diwani wa Kata hiyo Alhaji Omari Kariati amewasaidia kuwafungia umeme wa jua hivyo kupunguza tatizo hilo.

'' Umeme wa jua tulio fungua unawasha taa nne za vyumba vyotev pamoja na nje hivyo imetusaidia sana kwani awali tulikuwa tukilazimika kutumia vibatali kumulikia wakati wakina mama wakijifungua" alisema Belindani.

Alisema changamoto nyingine ambayo ni kubwa ni ukosefu wa vitanda vya kujifungulia ambapo katika kituo hicho kipo kimoja na kuleta usumbufu pale inapotokea wajawazito zaidi ya wawili wanahitaji kujifungua

Alisema tatizo lingine ni ukosefu wa maji salama ambapo hivi sasa wamalazimika kutumia ya visima jambo linalowafanya wakazi wengi wa Kata hiyo kusumbuliwa na magonjwa ya matumbo.

Mwenyekiti wa Kata hiyo Hamza Said alisema ili kukabiliana na tatizo la maji lilidumu kwa zaidi ya miaka 20 wamenununua mabomba na mashine ya kusukuma maji kwa kishirikiana na Diwani wao Alhaji Omari Kariati na kwamba muda si mrefu wananchi wa Kata yake watapata maji salama

Alisema tayari wamekwisha nunua mabomba ya chuma na pampu ya kusukuma maji wanachosubiri ni mafundi kuanza kazi ya kufunga vifaa hivyo na kuwa mara baada ya kuanza kutoka maji wananchi watachangia kununua ndoo moja kwa sh.20,000 na kuwa vifaa hivyovimenunuliwa kwa thamani ya zaidi ya sh. milioni moja

Alisema umeme huo wa jua waliofungiwa na Diwani wao katika Kituo chao cha Afya umegharimu sh.427,000 na utasaidia kuweka usalama wa kituo hicho

Akizungmzia katika suala la maebndeleo ya elimu alisema Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa Benard Membe wameisaidia Kata hiyo vifaa vya ujenzi wa madarasa mawili ya Shule ya Msingi ya Kwadelo kwa kuoa mabati 76 na Diwani wao ameahidi kutoa mabati 24 ili kuongezea nguvu ya uharakishaji wa vyumba hivyo pamoja na kumunua kitanda cha kujifungulia wajawazito chenye thamani ya sh 560,000.

Akiabidhi msaada wa mabati hayo kwa niaba ya Mawziri hao Diwani wa Kata hiyo Alhaji Omari Kariati katika hafla ya maafali ya nane ya Shule ya Msingi ya Kwadelo ambapo alikuwa mgeni rasmi aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni badala ya kuwaacha wakizurura mitaani.

“Rais wetu Jakaya Kikwete ameanzisha vyuo vikuu vingi na sekondari za kata kwa ajili ya kusoma watoto wetu tusimuangushe watoto wapelekwe shuleni kwani ametekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), alisema Kariati

Alisema haipendezi kuona watoto wanaonelana walipita mitaani hasa mijini wakiombaomba wakati wazazi wao wanauwezo wa kuwasaidia kuwasomesha kwa kupitia kilimo na shughuli zingine mbalimbali.

Katika ziara hiyo pamoja na kuwa mgeni rasmi Diwani huyo alikagua shughuli za maendeleo kukamilika kwa umeme wa jua katika Kituo cha Afya cha Kata hiyo, vifaa vya ufufuaji wa miundombinu ya maji pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya katika Kijiji cha Makirinya.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....