Tuesday, September 18, 2012

LASABA KUFANYA MITIHANI KESHO

0 comments

 Na mwandishi wetu IRINGA
Mikoa ya Iringa na Njombe imejipanga kuhakikisha kuwa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2012 inafanyika katika hali nzuri na kutokuruhusu mianya yoyote ya udanganyifu na kusababisha kufutiwa kwa matokeo kwa baina ya shule za msingi.

Akifafanua maandalizi ya mitihani hiyo ofisini kwake, Afisa Elimu Mkoa wa Iringa, Mwalimu Joseph Mnyikambi aliyepewa pia jukumu la kusimamia mitihani hiyo kwa mikoa ya Iringa na Njombe amesema kuwa tayari semina zimeendeshwa na kamati ya usimamizi wa mitihani ya mkoa katika Halmashauri zote nane za mikoa ya Iringa na Njombe. Amezitaja Halmashauri hizo kuwa ni Njombe, Mufindi, Makete, Ludewa, Kilolo, Iringa, Njombe Mji na Iringa Manispaa.

Akiongelea maandalizi amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na leo ndiyo siku ya kuwapeleka wasimamizi katika vituo vyao ya kusimamia mitihani hiyo. Amesema “kwa mujibu wa sheria zetu huwezi kumwambia msimamizi atasimamia wapi mtihani huo”. Amesema kuwa lengo ni kuzuia udanganyifu na hongo kutoka kwa jamii kwenda kwa msimamizi na kutoka kwa msimamizi kwenda kwa jamii pamoja na wanafunzi.

Kuhusu taratibu, Mwalimu Mnyikambi amesema kuwa taratibu ni za kawaida na zilizozoeleka isipokuwa kitu kipya ni mwaka huu watahiniwa wote watatumia penseli na fomu maalumu kujibu mitihani hiyo kwa kusiliba kwa sababu kwa mara ya kwanza itatumika teknolojia mpya ya ‘optical mark reader’ (OMR). Amesema kuwa majibu yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta.

Amesema kuwa mitihani hiyo itafanyika kwa siku mbili na itaanza kesho tarehe 19 -20 Septemb, 2012. masomo yatakayotahiniwa ameyataja kuwa ni Sayansi, Hisabati na Kiswahili. Mengine ni Kiingereza na Maarifa ya Jamii.

Ni kwa namna gani mkoa umejipanga kukabiliana na udanganyifu unaoweza kusababisha wanafunzi kufutiwa matokea, Afisa elimu mkoa wa Iringa amesema “kama mkoa tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa udanganyifu haufanyiki katika mikoa ya Iringa na Njombe kwa kuzingatia taratibu zote za mitihani”. Ameitaja miongoni mwa mikakati hiyo kuwa ni pamoja na kila mwanafunzi kukaa katika dawati lake na kukaa mmoja ili kuondoa uwezekano wa kutizamiana. Amesema katika semina kwa wasimamizi wa mitihani, msisitizo ulikuwa ni kuhakikisha hakuna udanganyifu wowote utakaopewa nafasi katika mtihani huo ili kuhakikisha kila mwanafunzi anayeingia kidato cha kwanza anajua kusoma na kuandika na anakwenda kwa kufaulu vizuri.

Mwalimu Mnyikambi ameitaja idadi ya wanafunzi watakaofanya mitihani hiyo ya kumaliza elimu ya msingi kwa mikoa ya Iringa na Njombe kuwa ni 43,499 kati yao wasichana ni 23,015 na wavulana ni 20,484. amesema jumla ya shule zote ni 887. Na. Dennis Gondwe, IRINGA
Zaidi ya wanafunzi 43,000 wanatarajia kufanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kwa mikoa ya Iringa na Njombe  mwaka huu na maandalizi ya mitihani hiyo yamekamilika.

Katika taarifa kwa vyombo vya habarrí iliyotolewa na Afisa Elmu Mkoa wa Iringa Mwalimu Joseph Mnyikambi mwwenye dhamana ya kusimamia mitihani hiyo kwa mikoa ya Iringa na Njombe amesema kuwa jumla ya wanafunzi 43,499 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika mikoa hiyo mwaka 2012. amewata wanafunzi hao kuwa wasichana ni 23,015 na wavulana ni 20,484.

Ameitaja idadi ya wanafunzi hao na Halmashauri wanazotoka kuwa ni Iringa 7,043, Kilolo 5,554, Ludewa 3,933, Makete 2,929, Mufindi 8,350, Njombe 9,007, Njombe Mji 3,511 na Iringa Manispaa ni 3,169. Akiongelea aina za watainiwa wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kuwa ni mfumo wa kiswahili wanafunzi 42,947, uono hafifu 14 wasioona 11 na ‘english medium’ 527.

Akiongelea maadalizi ya mitihani hiyo itakayoanza tarehe 19-20 Septemba, 2012, Mwalimu Myinkambi amesema kuwa maandalizi yote ya msingi yamekamilika na wasimamizi wamepatiwa mafunzo yaliyoendeshwa na Kamati ya Usimamizi wa mitihani ya mkoa katika Halmashauri zote nane.

Afisa Elimu Mkoa wa Iringa amesema kuwa mikoa hiyo imejipanga vizuri kuhakikisha mitihani hiyo inafanyika katika hali inayokubalika. Amesema katika mafunzo kwa wasimamizi wa mitihani hiyo wamesisitizwa kuhakikisha wanasimamia kwa umakini mkubwa na kutoruhusu Mwanya wa udanganyifu wa aina yoyote na kufuata taratibu zote za mitihani. Amesema ili kuhakikisha kuwa hakuna kutazamiana baina ya wanafunzi, kila mwanafunzi atakaa katika dawati lake. Amesema endapo itatokea shule au wanafunzi kuhusika katika udanganyifu katika mitihani hiyo, msimamizi atawajibika kwa uzembe huo.

Amesema tofauti na siku za nyuma, katika kipindi hiki kutakuwepo na wafuatiliaji mbalimbali ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi na baraza la mitihani la Taifa.

Amesema kuwa lengo la kuweka umakini mkubwa katika mitihani hiyo ni kuondokana na aibu ya baadhi ya wanafunzi kufaulu kujiunga na kidato cha kwanza pasipo kujua kusoma na kuandika.

Mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2012 itafanyika kwa siku mbili na itaanza kesho tarehe 19 -20 Septemba na masomo yatakayotahiniwa ni Sayansi, Hisabati na Kiswahili. Mengine ni Kiingereza na Maarifa ya Jamii.

Ikumbukwe kuwa mitihani ya mwaka huu, watahiniwa wote watatumia penseli na fomu maalumu kujibu mitihani hiyo kwa kusiliba kwa sababu kwa mara ya kwanza itatumika teknolojia mpya ya ‘optical mark reader’ (OMR). Amesema kuwa majibu yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....