Friday, September 7, 2012

MAANDAMANO YA WAISLAM DAR: SERIKALI YATOA TAMKO

0 comments

TAMKO LA AWALI LA SERIKALI JUU YA RISALA YA WAISLAM KWA MHESHIMIWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ILIYOTOLEWA NA KATIBU MKUU WA MAMBO YA NDANI YA NCHI TAREHE 07 SEPTEMBA, 2012

KUTOKANA NA MHESHIMIWA WAZIRI NA NAIBU WAKE KUWA NJE YA OFISI, KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI AMEPOKEA RISALA YA WAISLAMU NA KWAMBA ATAIFIKISHA KWA WAZIRI MARA TU ATAKAPORUDI NCHINI.

KATIKA MAZUNGUMZO KUNA MANENO KUWA KUNA WAISLAMU WAMEWEKWA NDANI KUTOKANA NA ZOEZI LINALOENDELEA LA SENSA.  KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, AMETOA AMRI KWA RPC WOTE KUSITISHA UKAMATAJI WA WATU KUTOKANA NA ZOEZI LA SENSA NA KWAMBA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAACHIWE KWA DHAMANA.

MAMBO MENGINE YOTE YALIYOTAJWA KWENYE RISALA YA WAISLAMU YATASHUGHULIKIWA MARA BAADA YA WAHESHIMIWA MAWAZIRI WENYE DHAMANA HIYO KURUDI NA MTAJULISHWA.

TAMKO LIMETOLEWA NA,
                             
MBARAK M. ABDULWAKIL
KATIBU MKUU
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
07 Septemba, 2012

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....