Sunday, September 30, 2012

MWINYI: MAANDAMANO SIYO NJIA SAHIHI YA KUSAKA MAENDELEO

0 comments
* Asema, njia sahihi na ya uhakika ni kuchangamkia fursa na kufanya kazi kwa bidii
NA BASHIR NKOROMO, DAR ES SALAAM
RAIS Mastaafu Ali Hassani Mwinyi amesema kufanya maandamano siyo njia ya uhakika  ya kufikia malengo wanayotaka wananchi  katika kutafuta maendeleo.
       Amesema, njia sahihi na ya uhakika ni kujituma na kufanyakazi kwa bidii  kwa kuzitumia fursa zilizopo ili  kuwapata maendeleo kwa mtu mmoja moja, jamii  nchini na duniani kote kwa jumla.
      Mwinyi amesema hayo leo, katika hafla ya kuwakabidhi tangi kubwa la maji na kitanda cha kujifungulia, wananchi wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa mkoa wa Dodoma, iliyofanyika nyumbani kwake, Mikocheni mjini Dar es Salaam.
       Pamoja na kukabidhi vifaa hivyo, Mwinyi aliwahimiza Vijana wa Kata hiyo, kwenda kulima huko kwao, kutokana na uongozi wa kata hiyo, kutangaza fursa ya kumpatia kila kijana shamba hekari tano ambalo atalimiwa kwa trekta kwa mkopo.
      Mapema, Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati, alimwambia Mwinyi, kwamba, uongozi wa kata hiyo umetotoa ofa kwa vijana kwenda kulima huko, na watapatiwa ekari tano kila mmoja na kisha kulimiwa kwa mkopo kwa kutumia trekta 64 ambazo tayari zipo.
    Kariati alisema, kwa ekari hizo kijana anaweza kuvuna gunia 100 za alizeti au ufuta na kwamba na mkopo wa kulimiwa ataulipa kwa kutoa magunia matano tu na kubakiwa na gunia 95 ambazo zitampatia mamilioni ya fedha.
    Alisema tayari vijana 50 wanaofanya shughuli mbalimbali ikiwemo biashara ndogondogo jijini Dar es Salaam, wameshajiorodhesha kwenye kushiriki kilimo hicho.
        "Hivi sasa Tanzania tunaishi katika mazingira magumu kidogo, vitu na usafiri vinapanda bei kutokana na bei ya mafuta kuwa kubwa hata kimataifa, Vijana hawana ajira, tena si Tanzanaia tu hata huko mnasikia vijana wanafanya maandamano katika nchi kadhaa, kushinikiza serikali zao ziboreshe hali ya maisha", alisema Mzee Mwinyi na kuongeza.
         "Hata hivyo maandamano hayawezi kuwa suluhisho la uhakika la dhiki hizi ila kujituma kufanyakazi kwa kuzitumia fursa zilizopo. Sasa Vijana wa Kwadelo itumieni fursa hii mjikomboe kiuchumi".
       Mbali na kukabidhi tangi na kitanda ambavyo vimetolewa kwa ushirikiano wa Waziri wa Mambo ya nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Mwinyi alikabidhi pia sh. 200,000 kwa kijana  KIasim Athumani, wa Kwadelo kwa ajili ya masomo ya ualimu anayoendelea nayo katika Chuo Cha Ualimu  Ununio, Bagamoyo mkoa wa Pwani.
        Wakati kitanda ambacho gharama yake ni sh. 700,000 kitatumika katika zahanati ya Kwadelo, tangi la maji lenye dhamani ya sh. 650,000, litatumika kuwapatia maji safi na salama wakati wa kijiji cha Kerereng'ombe katika kata hiyo.ho. PICHA KIBAO ZA TUKIO HILO BOFYA HAPA

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....