Thursday, September 20, 2012

NAIBU WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA ATEMBELEA BAADHI YA MAHAKAMA

0 comments
 Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Kisarawe lililopo Kisarawe mjini Mkoani Pwani. Jengo hili ni la kisasa ambalo lina korti mbili, mahabusu ya wanawake na ya wanaume, vyoo vya ndani na nje, stoo na ofisi mbalimbali.
 Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Abdala A. Pendekezi (wa pili kulia) akimwonesha kiwanja kitakachojengwa Mahakama ya Mwanzo Kimanzichana Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Jasmine Kairuki (wa kwanza kulia) alipofanya Ziara ya Siku moja ya kutembelea Mahakama nchini. Wa kwanza Kushoto waliosimama mbele ni Naibu MKurugenzi wa Mahakama za Mwanzo Mh. Warsha Numbu, anayefuatia nI Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Sila.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Jasmine Kairuki akipata maelezo  kutoka kwa  Kaimu Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mh. Jaji Mmila alipofanya ziara ya kikazi jana (20/09/2012) ya kutembelea baadhi ya Mahakama nchini ikiwemo Mahakama Kuu ya Tanzania, Mahakama ya Mwanzo Kimanzichana, Mahakama ya Wilaya Kisarawe na Mahakama ya Mwanzo Kibaha Maili Moja.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....