Wednesday, September 12, 2012

RAIS KIKWETE AANZA ZIARA NCHINI KENYA

0 comments
 Rais Jakaya Kikwete akipokewa rasmi na Rais Mwai Kibaki wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya Rais Kikwete kuwasiri kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Kenya tarehe 11-13.9.2012.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua  mara baada ya kuwasiri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta akiambatana na Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Kenya tarehe 11.9.2012.
 Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa  kwenye mapokezi yake mara baada ya kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta nchini Kenya kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
 ‘Angalia kiatu Mheshimiwa’  Rais Mwai Kibaki anaonekana akimwambia mgeni wake Rais Kikwete wakati wakiangalia ngoma ya utamaduni iliyokuwa ikichezwa na wananchi wa kabila la Wakurya wa nchini Kenya wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete na ujumbe wake kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta tarehe 11.9.2012.
 Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo ya kiserikali kati yake na mwenyeji wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya yaliyofanyika ikulu huko Nairobi katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu nchini Kenya tarehe 11.9.2012.
 Rais Jakaya Kikwete akizindua rasmi jengo la Kenyatta University School of Hospitality and Tourism jijini Nairobi katika siku ya kwanza ya ziara yake nchini Kenya tarehe 11.9.2012.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Kilonzo Musyoka wakati wa dhifa ya taifa iliyoandaliwa na Rais Mwai Kibaki jijini Nairobi tarehe 11.9.2012.
Rais Jakaya Kikwete akigonganisha glasi za kinywaji na Waziri Mkuu wa Kenya Mheshimiwa Raila Odinga wakati wa dhifa ya kitaifa aliyofanyiwa na mwenyeji wake Rais Mwai Kibaki wa Kenya katika siku ya kwanza ya ziara ya kiserikali anayoifanya nchini humo tarehe 11.9.2012. PICHA NA JOHN  LUKUWI

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....