Friday, October 5, 2012

ZIARA YA RAIS KIKWETE, MAREKANI

0 comments
 Pichani ni  Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati, Rais alipokwenda Ofisini kwa Ban Ki Moon hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  ilikuwa muda mfupi kabla ya  uzinduzi wa awamu ya pili ya ufadhili wa uboreshaji wa huduma za afya ya mama na mtoto.
 Rais  Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni Ofisini kwai Katibu Mkuu  wa Umoja wa Matifa, Ban Ki Moon
Meya Michael Bloomberg, Ban Ki Moon, Rais  Jakaya Kikwete na Dr. Hellen wakiangalia video fupi iliyokuwa ikionyesha kazi zilizofanywa za ukoaji wa  akina mama wajawazito kwa kuwapatia huduma ya upasuaji wa dharura, huduma ambayo imepatika kwa ufadhili wa  Meya na   Philanthropies Michael Bloomberg ambapo kwa kupitia ufadhili alioufanya kuanzia mwaka 2006 zaidi ya wataalam 106 wakiwamo wakunga na manesi wamepatiwa mafunzo ya upasuaji wa dharura, pia huduma za afya zimeboreshwa kwa kujenga au kuvifanyia ukarabati vituo vya afya na zahanati katika ngazi za vijiji katika  maeneo ya  mikoa ya Pwani, Morogoro na Kigoma. Ufadhili  na kazi kubwa iliyofanywa na  Bloomberg   pamoja na juhudi za   Rais Jakaya Kikwete zimemvutia Dr. Hellen naye kuwekeza nchini Tanzania.
Rais  Jakaya Kikwete akiongoza ujumbe wa Tanzania katika  mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki  Moon ambaye naye aliongoza ujumbe wake. Matukio hayo yote yamefanyika siku ya  Jumanne katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa,  Jijini New York, Marekani

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....