Monday, November 26, 2012

JK AAPISHA MAJI WAWILI

1 comments

DAR ES SALAAM, TANZANIA
RAIS Jakaya Kikwete amewaapisha majaji wawili wa mahakama ya rufani na  kuwataka wananchi kupima uwezo wao kwa kufanyia tafiti hukumu wanazozitoa badala ya kusikiliza maneno ya mtaani.

Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya wanasiasa kudai kuwa majaji wanaoteuliwa na Rais Kikwete hawana uwezo kitaaluma hivyo wanatoa hukumu zisizo stahili.

Majaji hao waliapishwa leo Ikulu, Dar es Salaam na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo mawaziri na watendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Wakizungumza baada kuapishwa majaji hao waliahidi kutotoka nje ya viapo vyao. majaji hao ambao ni Bethewel Kasefu Mmilla na Ibrahim Hamisi Juma, walisisitiza kufanya kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia maadili na kiapo cha kazi hiyo.

Jaji Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya sheria na Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania Dar es Salaam alisema nafasi hiyo ni changamoto kwake katika kutekeleza kazi ambazo zinahitaji kuzingatia zaidi sheria.
Kuhusu suala la uwezo wa hukumu wanazozitoa aliwataka wananchi kutosikiliza maneno ya mtaani bali wapime hukumu wanazozitoa kwa kuzifanyia tafiti na kufuatilia mienendo ya kesi.

Alisema tatizo la ucheleweshwaji wa kesi linasababishwa na mambo mengi likiwemo la upungufu wa majaji na mahakimu.

Kwa upande wake Jaji Mmilla ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, pia alisema atafanya kazi kwa kuzingatia maadili ili kuhakikisha kila mwananchi anaefikishwa katika vyombo vya sheria anapata haki yake kwa kulingana na kosa alilolifanya.

Pamoja na kuapishwa kwa majaji hao, Pia Rais Kikwete aliwaapisha watumishi wengine wawili ambao ni Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jaji John Mkwawa na Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria, Winfrida Koroso.

Kwa upande wake Mkwawa alisema nafasi hiyo ameteuliwa kwa mara ya pili hivyo changamoto alizoziona awali ndani ya tume hiyo ataandaa mikakati ya kukabiliana nazo katika awamu hii.

“tumekumbana mambo mengi  katika kipindi cha uchaguzi mkuu hivyo ili kufanikisha kuboresha utendaji kazi wa tume hii tumeandaa bajeti ya mabilioni ya fedha ambayo yatasaidia kusaidia kuboresha kazi za tume hii,” alisema.

Kwa upande wake Winfrida alisema katika nafasi aliyoteuliwa atahakikisha anasimamia vyema mabadiliko ya sheria ambazo zinalalamikiwa na wananchi kama vile sheria za migogoro ya ardhi na madai.

1 comments:

Anonymous said...

Неllo! I've been following your weblog for a long time now and finally got the courage to go ahead and give you a shout out from Austin Tx! Just wanted to say keep up the excellent work!

my site: personal loans

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....