Sunday, November 4, 2012

SIMBA YALIZWA 2-0 MORO, YANGA YANG'AA 2-0 DAR

0 comments

Katika mechi zilizopigwa kwenye Viwanja Tofauti, zikihusisha timu za Yanga na Simba, zimemalizika huku Yanga wakichekelea baada ya kupata mabao 2-0 dhidi ya  Azam katika mechi ya timu hizo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Lakini kwa upande wa Simba iliyokuwa ikinyukana na Mtibwa imesababisha mashabiki wake kunyong'onyea baada ya kupata kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Wakata miwa wa Mtibwa al maarufu Mtibwa Sugar, katika mechi ya timu hizo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....