Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Jambo Leo, Julius Kihampa akimvisha pete ya ndoa Mtangazaji Shirika la Utangazaji la Taifa, Grace Kingarame wakati wa kufunga pingu za maisha kwenye Kanisa la Anglikana la St Albano Dar es Salaam.
                 Grace Kingarame akimvisha pete mumewe Julius Kihampa mbele ya Padi Cosmas Mhina
                                                      Kihampa na mkewe Grace Kingarame
                                                    Ibada ya kuwafungisha ndoa ikiendelea
     Kihampa akimvua shela la kichwani Grace
 Kihampa akila kiapo cha uaminifu cha ndoa mbele ya mkewe Grace. Kulia ni Patroni wake Chacha Maginga na Matroni Levina
                    Grace Kingarame akila kiapo cha uaminifu cha ndoa mbele ya mumewe na kanisa
 Padri Cosmas Mhina akiwafungisha ndoa Kihampa na Grace
                                                                  Kwaya ya kanisala hilo ikitumbuiza
                              Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wakishuhudia ndoa hiyo ikifungwa
                                                   Baadhi ya wapambe wa harusi hiyo
                                         Padri akiwaelekeza jinsi ya kupiga saini hati ya ndoa
                                         Kihampa na Grace wakikabidhiwa hati za ndoa
                                Wanandoa hao wakiwa na furaha huku wakionesha hati za ndoa yao
 Bwana harui Julius Kihampa akiwa amejiinamia akitafakari jinshi ya kukabiliana na maisha mapya ya ndoa
                                         Maharusi wakitoka kanisani baada ya kufunga ndoa
                                                                    Kweli wanameremeta
                                     Maharusi wakipanda kwenye Lemousine lililoandaliwa kwa ajili yao
Msafara wa maharusi hao ukiondoka kanisani kuelekea Coco Beach. Kamanda wa Matukio Blog inaahidi kuendelea kuwaletea matukio zaidi ya harusi hiyo, wakiwa Beach na Reception. (PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)