Tuesday, June 4, 2013

Kesi dhidi ya Pistorius yaakhirishwa

0 comments

Pistorius anakana kumuua mpenzi wake Reeva kwa maksudi nyumbani kwake
Kesi inayomkabili mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius Imeakhirishwa na mahakama hadi tarehe 19 mwezi Agosti.
Pistorius, alirejea mahakamani hii leo baada ya kupewa dhamana wakati kesi yake iliposikilizwa mara ya kwanza mapema mwaka huu.
Oscar anakabiliwa na kesi ya mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp nyumbani kwake mwezi Februari.
Anakanusha madai ya kumuua mpenzi wake kwa maksudi akisema alikosea kwa kudhani kuwa alikuwa jambazi kavamia nyumba yake.
Viongozi wa mashtaka wameomba muda zaidi kuweza kukusanya ushahidi dhidi ya mwanariadha huyo aliyeshiriki michezo ya Olimpiki mjini London.
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg anasema kuwa ushahidi mwingi katika kesi hiyo utatokana na uchunguzi wa kisayansi unaofanywa ndani ya bafu ambamo Reeva Steenkamp aliuawa.
Kesi hiyo kwa upana wake huenda isianze kusikilizwa hadi mwaka ujao.
Mwanariadha huiyo alichiliwa kwa dhamana na amekuwa akiishi katika nyumba ya jamaa wake mjini Pretoria.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....