Tuesday, June 25, 2013

JARIDA LAMTAJA MOHAMMED DEWJI KUWA MJASIRIAMALI KIJANA MWENYE MAFANIKIO YA KIPEKEE AFRIKA

0 comments
BNlXP2uCQAAypL0
Na Mwandishi Wetu
Mjasirimali mchapakazi na Mbunge Kijana nchini Tanzania, Mohammed Dewji (MO) ametajwa katika jarida la Kimataifa la mabilionea duniani katika Nyanja za biashara (Forbes Africa Magazine) kama mjasirimali mwenye umri mdogo mwenye mafanikio ya kuigwa hapa Afrika na duniani kwa ujumla taarifa la Jarida hilo limeeleza.
      Kwa mujibu wa Jarida hilo la Forbes African Magazine MO   amekuwa Mtanzania wa Kwanza kupata kuhojiwa na (Forbes Magazine) mafaniko, changamoto na matatizo kadhaa kwenye uwanja wa biashara kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki na kati.
    Mo akihojiwa na Jarida hilo alisema toka kwenye masaa mia moja kwa wiki na kutengeneza faida ya Millioni 85 dola za kimarekani! Ni mafanikio makubwa katika biashara Afrika.
     Anasema ni safari ya takribani miaka 12 ya ushindani wa kibiashara ndani ya mipaka ya Tanzania na Afrika kwa ujumla.
    “Nani anaweza kufikiri kwamba tunaweza kubadilisha biashara yetu toka Millioni 50 za kimarekani hadi dola Billioni 2.1 ndani ya miaka 12 tu,’ alinukuliwa akisema.

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....