Thursday, August 29, 2013

IGP SAIDI MWEMA APANGUA MAKAMANDA KADHAA

0 comments
IGP SAID MWEMA
 DAR ES SALAAM, Tanzania
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Mikoa na Vikosi.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mwarakibu Mwandamizi Advera Senso, imesema mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara  Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi  na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Stephen  kutoka Makao Makuu ya Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi  Viwanda vya ndege Kamishina Msaidizi (ACP) Deusdedit  Kato amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi  na nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishina  Msaidizi wa Polisi (ACP) Selemani Hamisi kutoka Makao Makuu Idara ya Upelelezi.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad anayeenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Viwanja vya ndege ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na David Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).

"Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi" imesema taarifa hiyo. theNkoromo Blog

0 comments:

Post a Comment

Mdau mtandao huu ni kwa ajili yako, weka maoni yao uelimishane na wenzako, Zingatia kutoleta maoni yanayochafua hali ya Hewa! Sasa Endelea....